Hatua za kufuata
    • 1
      Chagua huduma ya kuomba umeme
    • 2
      Chagua Dhumuni, Aina ya ombi, Aina ya muombaji, Aina ya kitambulisho/utambulisho wa mlipa kodi na Namba ya kitambulisho/utambulisho
    • 3
      Tumia namba ya kitambulisho cha Taifa kwa ombi lililokusudiwa kwa madhumuni ya makazi na fuata muundo huu: 1984081911660000xxx
    • 4
      Tumia namba ya usajili wa kampuni/TIN kwa Kampuni au Taasisi
    • 5
      Bonyeza/bofya Anzisha ombi jipya
    • 6
      Jaza wasifu, mawasiliano mbadala na maelezo ya makazi
    • 7
      Bonyeza/bofya tuma ombi
    • 8
      Utapokea ujumbe baada ya kujaza maelezo kwa ukamilifu na kufanikiwa kutuma
    • 9
      Tafadhali bonyeza/bofya hapa kuona orodha ya wakandarasi wa umeme wanaostahili au tembelea ofisi zao
    • 10
      Mpatie mkandarasi uliyemchagua namba ya ombi uliyopatiwa kutoka kwenye mfumo na namba ya simu uliyotumia kuombea umeme ili kumuwezesha kujaza maelezo ya mfumo wa mtandao wa nyaya katika jengo/eneo lako kwenye mfumo wa maombi mtandaoni
    • 11
      Mkandarasi wa umeme atajaza maelezo ya mtandao wa nyaya na tamko lake na kutuma maelezo ya muombaji TANESCO kupitia mfumo wa maombi mtandaoni
    • 12
      Muombaji utajulishwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) moja kwa moja baada ya mkandarasi wa umeme kutuma maelezo yake ya mfumo wa mtandao wa nyaya kwenye jengo/eneo lako TANESCO
    • 13
      TANESCO itafanya upimaji katika eneo la mteja ili kubaini gharama na mahitaji ya kuunganishiwa umeme baada ya hapo mteja atapatiwa makadirio ya bei na namba ya kulipia ili afanye malipo kupitia ujumbe mfupi wa maandishi(SMS) moja kwa moja au kupitia kupakua kutoka kwenye tovuti ya maombi ya umeme TANESCO
    • 14
      Mteja atalipia kupitia njia mbalimbali za malipo
    • 15
      Mteja atajulishwa moja kwa moja kupitia mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) baada ya kufanikiwa malipo yake
    • 16
      TANESCO itaunganisha umeme kuangaza maisha ya mteja